RC Kilimanjaro ajitokeza kumtetea aliyedaiwa kufumaniwa

26May 2020
Na Mwandishi Wetu
KILIMANJARO
Nipashe
RC Kilimanjaro ajitokeza kumtetea aliyedaiwa kufumaniwa

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Anna Mghwira, Mwanaharakati, Joyce Kiria pamoja na Diwani wa Boma Mbuzi Moshi, Juma Raibu wamejitolewa kumsaidia kupata matibabu mwanamke aliyepigwa na kuumizwa na video kusambaa kwenye mitandao ya kijamii akidaiwa kufumaniwa na mume wa mtu.

Venna Kimaro.

Wakiwa nyumbani kwa mwanamke huyo Venna Kimaro, RC Mghwira ameagiza mwanamke huyo kupelekwa Hospitali ya Rufaa Mawezi kwa ajili ya kupatiwa matibabu na kumuagiza Mganga Mkuu wa hospitali hiyo kumuhudumia mpaka atakapopona.

 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro limewataka watuhumiwa waliohusika kutenda tukio hilo kujitokeza kwani hilo ni tuko la jinai na msako wa kumtafuta na mwanamke huyo na wenzake unaendelea.

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro amewataka Wanawake kuacha tabia ya kuisi wanawake mwezao kwamba muda wote wakiwa na wanaume wanaendekeza mapenzi kwani kilicho tokea kwa mwananchi huyo sio fumanizi bali ni mazungumzo ya kibiashara.

Habari Kubwa