RC Kunenge aahidi kushughulikia umeme kwenye viwanda

26Jan 2022
Julieth Mkireri
PWANI
Nipashe
RC Kunenge aahidi kushughulikia umeme kwenye viwanda

MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge ameahidi kushughulikia suala la umeme kwenye viwanda ili kuwawezesha wawekezaji kutimiza malengo ya uzalishaji kwenye viwanda vyao.

Kunenge ametoa ahadi hiyo alipokuwa katika ziara yake ya kikazi kukagua hali ya uzalishaji kwenye viwanda vya Kampuni ya Lake vilivyopo Kibaha.

Akiwa katika viwanda hivyo alielezwa kuhusiana na umeme mdogo ambao haukidhi mahitaji ya uzalishaji ambapo aliahidi kuendelea kufuatilia suala hilo ambalo tayari ameanza kulishughulikia.

Kunenge amesema tayari amewasilisha kero hiyo kwa Waziri wa Nishati na ataendelea kulifuatilia ili kupata utatuzi wake na kuwawezesha wawekezaji kutimiza malengo yao.

Katika ziara hiyo Kunenge ametembelea kiwanda cha kutengeneza matenki ya magari ya mafuta ambacho ni cha kwanza kwa Afrika Mashariki.

Kiwanda kinginge kinachomilikiwa na kampuni ya Lake kilichopo Kibaha ni cha kutengeneza matenki ya maji, mabomba ya plastiki na kiwanda cha mitungi ya gesi na kiwanda cha gypsum.

Kinenge amempongeza mwekezaji huyo mzawa kwa uwekezaji wake mkubwa ambao umewezesha zaidi ya ajira 400.

Afisa muajiri wa Lake group Fadhil Msemwa ameshukuru mkuu wa mkoa kwa ziara yake ya kusikiliza kero za wawekezaji na kuomba ziara hizo ziwe endelevu kwani zinawapa motisha kuona namna Serikali inavyowajali.

Habari Kubwa