RC Luhumbi aagiza ujenzi wa zahanati vijiji 74

17Jun 2021
Neema Emmanuel
MWANZA
Nipashe
RC Luhumbi aagiza ujenzi wa zahanati vijiji 74

MKUU wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi ameagiza ujenzi wa zahanati kwa vijiji  74 vilivyopo wilayani Kwimba,mkoani Mwanza visivyokuwa na huduma hiyo zijengwe ili wananchi wapate huduma kwa kila Kijiji.

MKUU wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi.

Hayo ameyabainisha leo mara baada ya kupitia hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2019 hadi 2020, ambapo amewaagiza maofisa tarafa kwenye maeneo yao waitishe kikao na watendaji wa kata na vijiji ili kila kijiji kipate ramani na wajilidhishe na eneo ili zoezi la ujenzi wa msingi wa zahanati kwa kila kijiji uanze.

"Naomba muyabebe haya maagizo kwa sababu nyie ndio mnaomsaidia mkuu wa wilaya kwenye kata zenu, tutafute mchanga na mawe na mimi nitakuja kuzunguka kata zote tunataka mwaka 2025 wakati Katibu wetu wa chama anasimama kwenye jukwaa anawanadi madiwani awe anasema tuliahidi tunatekeleza," amesema na kuongeza;

"74 ni idadi kubwa  mno huko nilipotoka kazi imeanza maboma yanakwenda kwa hatua mbalimbali,nimetoka Buchosa wanaupungufu wa zahanati  24, Sengerema 30 hapa 70 vijiji vyote hivyo wananchi wanahitaji huduma nitakuja kwenye kata na tarafa zenu zote Mwenge wa Uhuru ukiondoka mimi naingia saiti tutakutana ili tujue kazi inaendeleaje tulishafanya majaribio hayo ikakubali na hapa itakubali,"ameeleza Mhandisi Luhumbi.

Aidha amewataka  wataalamu kuonesha  thamani ya fedha na wataetenda  kukagua majengo kama wamepigwa ama  hawajapigwa kwa sababu wanajua hiyo inatokana uzoefu,endapo kunamtu  mzembe asiyefanya kazi wamuweke pembeni kwani  maendeleo lazima  yaende mbele.

Habari Kubwa