RC Malima aifagiliaTBA

12Aug 2020
Renatha Msungu
Simiyu
Nipashe
RC Malima aifagiliaTBA

MKUU wa Mkoa wa Mara, Kigoma Malima, amesema Wakala wa Majengo nchini (TBA), wana uwezo wa kufanya mambo makubwa katika ujenzi, hivyo wanapaswa kuendelea kuboresha kazi yao kwa sababu serikali inawategemea.

Malima aliyasema hayo katika viwanja vya Nyakabindi, mkoani Simiyu wakati alipotembelea banda hilo.

"TBA wanamchango mkubwa katika ujenzi wa nchi hii kwa kujenga majengo yaliyo bora na kwa gharama nafuu," alisema Malima.

Hata hivyo, alisema mchango wa TBA bado unahitajika kwa sababu kuna maeneo mengi yanahitaji ujenzi ili kupendezesha maeneo.

"Kwa mfano hapa Simiyu bado kuna maeneo yanahitaji ujenzi hivyo wao wajipambanue kuhakikisha wanaboresha majengo na kuyajenga," alisema Kigoma.

Pia, alisema TBA bado ina mchango mkubwa katika suala la ujenzi hata wasipopewa majengo lazima waingie kama washauri katika kazi hiyo.

Alisema wanapaswa kuwa wabunifu katika kazi wanayoifanya na zabuni za ujenzi wanazochukua.

Akizungumzia mradi wa nyumba za makazi ya watumishi wa umma Bunking, alisema ni mradi wa gharama nafuu ambao unatekelezwa na TBA.

Alisema TBA ina kila sababu ya kujivunia kwa sababu inategemewa na kila mmoja hususani serikali ambayo nyumba na ofisi zake zinasimamiwa na TBA.

Alisema wanaimani na TBA ina uwezo wa kubadilisha maeneo kutokana ujenzi bora wanao ufanya katika maeneo mbalimbali.

Naye Kaimu Meneja Mawasiliano wa Umma na Masoko wa TBA Fredrick kalinga, alisema TBA ipo kwa ajili kujenga majengo bora ambayo yana sifa zote nchini.

Alisema wanajenga nyumba za gharama nafuu kwa jamii kwa sababu zinatoa msaada mkubwa.

Alisema wananchi na taasisi nyingine wasiwe na wasiwasi wanapokutana na TBA kila kitu kitakuwa sawa katika suala zima la ujenzi.

Aliongeza kuwa lengo lao ni kuona kila mmoja ananufaika na ujenzi wa nyumba hizo.

Akitoa mfano wa nyumba za gharama nafuu, alisema zipo katikati ya Jiji la Dar es Salaam na mradi huo una husisha nyumba 851 za makazi maduka, shule, migahawa ya kisasa na hoteli.

Kadhalika, alisema TBA inafanya kila kitu katika ujenzi na jamii, mteja anakuta nyumba iko tayari na yeye ni kuingia na kuishi.

"Naomba jamii ijitokeze kujengewa nyumba na TBA kwa sababu wanajenga nyumba bora," alisema Kalinga.

Habari Kubwa