RC Mongella apokea vifaa kinga corona

28May 2020
Neema Emmanuel
MWANZA
Nipashe
RC Mongella apokea vifaa kinga corona

Aga khan Development Network kwa ufadhili wa serikali ya watu wa Canada (Global Affairs Canada) kupitia mradi wa Improving Access to Reproductive Maternal and Newborn Health (IMPACT) Mwanza, watoa vifaa kinga vya maambukizi ya corona vyenye thamani ya Million 572,272,498.

Akizungumza baada ya kukabidhi vifaa kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, Meneja Mradi wa IMPACT Mwanza, Edna Selestine, amesema fedha hizo zimetolewa na wafadhili kwa ajili ya manunuzi ya vifaa tiba vitendea kazi pamoja na kuwezesha mafunzo ya watoa huduma za afya juu ya ugojwa wa corona pamoja na wahudumu wa afya ngazi ya jamii jinsi ya kuendelea kuelimisha jamii kuendelea kujikinga dhidi ya maambukizi.

Amesema vifaa hivyo vimenunuliwa kwa ushirikianao wa ofisi ya mganga mkuu wa mkoa wa Mwanza huku msaada huo ukiwalenga watoa huduma za afya na vituo vya kutolea huduma za afya mkoani humo ambao wamepongeza juhudi zilizofanywa na Rais Magufuli katika kukabiliana na maradhi hayo.

Ambapo siku ya leo wamemkabidhi vifaa vyevye thamani ya million 34,378,000 pamoja na mabegi ya wahudumu wa afya ngazi ya jamii yenye thamani ya 13,113,930 huku mradi ukiendelea na manubuzi ya vifaa tiba vyenye thamani ya takribani 295,000,000 na watavikabidhi pindi manunuzi yatakapokamilika na kupokelewa katika ofisi ya mradi Mwanza.

" Tunatambua kupitia Wizara ya Afya kuwa maambukizi ya ugonjwa wa corona yamepungua nchini pia tumehimizwa kuendeleza jitihada zote za kuendelea kujilinda mradi wa IMPACT utaendelea kushirikiana na mkoa kila inapowezekana ili kuhakikisha gonjwa hili linatokomezwa kabisa na afya za wananchi zinaendelea kuwa salama" amesema Selestine.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, akizungumza baada ya kupokea msaada huo amesema wamekuwa wabia na taasisi hiyo wameweza kujenga majengo 28 katika vituo vya afya vya sehemu mbalimbali kwa ajili ya huduma ya mama na mtoto pia vitanda 30 walivyotoa kwa ajili ya mapambano ya corona amevigawa 10 Ilemela,Nyamagana 10 na Buchosa 10.

Vilevile ameendelea kuwasihi wananchi kuendelea kufuata maelekezo ya wizara ya afya ,maombi,kutumia miti shamba iliyodhibitishwa sambamba na kupinga nyungu.

Habari Kubwa