RC Mwanza akomalia waliohusika upotevu wa milioni 353.2

17Jun 2021
Neema Emmanuel
MWANZA
Nipashe
RC Mwanza akomalia waliohusika upotevu wa milioni 353.2

MKUU wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel ametoa siku saba kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa mkoa huo kuwasilisha majina kwenye vyombo vya dola ya wakusanya mapato ya Halmashauri ya Sengerema waliohusika na upotevu wa zaidi ya milioni 353.2 ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

MKUU wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel.

Akizungumza wakati wa mkutano maalum wa baraza la madiwani wa mapitio ya hoja za CAG 2019 hadi 2020, amesema fedha hizo ambazo hazikupitishwa na kamati ya fedha zinahusishwa na wizi kwa kuwa wamefanya kinyume na taratibu hivyo ni lazima mkaguzi wa ndani wa mkoa kuwabaini waliohusika  kwenye maamuzi hayo.

Amesema hoja hiyo haitafugwa hadi fedha zitakaporejeshwe kwa sababu wametumia fedha ya ndani kinyume na utaratibu hivyo nakala hiyo ya mkaguzi ibainishe walipeleka wapi, nani alitoa kwa dokezo lipi, makusudio yapi na aliyefanya huo mchakato na zimefanya nini.

"Hii hoja haifutiki, fedha hii haijapelekwa lazima ipelekwe yote na wakaguzi mtusaidie hizi pesa ambazo kamati ya fedha haijahusika nani aliizinisha  walitumia kwa kitu gani, je hicho kitu walichokitumia kinauhalali wa baraza naomba kama hakuna uhalali wa baraza je zilitumika kwa nia njema kama hakuna nia njema hao watu wakamatwe warudishe fedha hizo popote pale walipo wawe hapa wawe wapi wakamatwe  hii pesa haitajiki kupotea haijahidhinishwa na kamati fedha ikatoka hii hoja mkaguzi naomba uje na maelezo huyu anakwenda polisi huyu yuko wapi au hela inarudishwa  "amesema Luhumbi.

Aidha amesema ni marufuku kutumia fedha yoyote ile bila kupitishwa na kamati ya fedha kwenye kikao halali pia kuanzia sasa fedha zote zinazopatikana taslimu waongee na benki  ziingie moja kwa moja hakuna mtu kugusa ili fedha  zote za maendeleo ziwe salama zipelekwe kwenye kazi iliyokusudiwa kwa wananchi kwa sababu kwa sasa inaliwa kutokana na kutopelekwa na kuonyesha picha ya  kuwa sisi hapo tupo kula hela kuliko kutatua kero za wananchi .

"Mnakopa million 300 hadi million 400 zahanati ,madarasa hakuna shida kwenye vijiji kwenye mitaa tunaelewana vizuri hii pesa lazima ipatikane ipelekwe kwenye vijiji na vyoona hapa kama sheria inasema peleka asilimia 40 unapeleka 10 tena kinyume na taratibu nini maana ya kuwa na baraza la madiwani kama fedha inapita kichocholo."ameeleza Luhumbi

Habari Kubwa