RC Sendiga atoa macho kwa wafanyabiashara wanaokimbia madeni

30May 2021
Na Mwandishi Wetu
Iringa
Nipashe Jumapili
RC Sendiga atoa macho kwa wafanyabiashara wanaokimbia madeni

​​​​​​​MKUU wa Mkoa wa Iringa, Queen Sendiga, ameigaiza Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoani humo kuwasilisha ofisini kwake majina ya wafanyabishara walioshindwa kulipa madeni yao baada ya makubaliano ya kisheria baina ya wafanyabiashara na mamlaka hiyo.

​​​​​​​Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Queen Sendiga.

Akizungumza kwenye kikao na wawakilishaji wa wafanyabiashara na machinga wa Mkoa huo amesema kuwa hatawafumbia macho wafanyabishara wote ambao tayari wamepewa maagizo ya kisheria kulipa madeni hayo lakini bado wamekuwa wanakaidi agizo hilo kutoka kwa mamlaka husika.

Akiwa katika kikao hicho Mkuu wa Mmkoa huo amemuagiza Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhakikisha anapeleka majina na kukutana na wafanyabiashara hao wanaokimbia kulipa madeni yao licha ya serikali kuagiza kulipa madeni hayo.

Habari Kubwa