RC Telack afungua milango ununuzi Almasi kwa njia ya mnada

21Feb 2020
Marco Maduhu
Shinyanga
Nipashe
RC Telack afungua milango ununuzi Almasi kwa njia ya mnada

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, amefungua milango kwa wazawa kununua madini ya Almasi kwa njia ya mnada kwa asilimia tano, ambayo uchimbwa katika mgodi wa Mwadui uliopo wilayani Kishapu mkoani humo.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akizungumza na wanunuzi wa madini ya Almasi katika mgodi wa Mwadui.

RC Telack amebainisha hayo leo wakati wa kutangazwa washindi wanne ambao wamefanikiwa kukidhi vigevyo vya kununua madini ya Almasi ya mgodi huo kwa njia ya mnada.

Amesema Serikali kwa kushirikiana na Wizara ya Madini na Tume ya Madini wanawakaribisha Watanzania wote, kununua Madini ya Almasi kwenye mgodi huo ili wapate kuinuka kiuchumi wa nchi.

"Zoezi hili la kutenda kununua Madini haya ya Almasi katika mgodi huu wa Mwadui lilianza februari 17 na leo Tarehe 21 tunatangaza washindi waliokidhi vigezo kununua madini ya Almasi,"amesema Telack na kuongeza kuwa;

Meneja Biashara na Mthamini wa Madini ya Almasi kutoka Tume ya Madini George Kaseza, akisoma washindi wanne ambao wamekidhi vigezo vya kununua madini hayo ya Almasi.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa.

"Pia natoa wito kwa wanunuzi hawa wadogo wa madini ya Almasi ambao mmeshinda kununua Almasi ya Mwadui mkauze kwenye masoko yetu ya madini pamoja na kulipa kodi ya Serikali," 

Aidha amesema kabla ya kutoanzishwa kwa masoko hayo ya Madini, Serikali ilikuwa ikikusanya kodi itokanayo na madini kiasi cha Shilingi Milioni 500, lakini baada ya masoko hayo wanakusanya Bilioni 10.

Naye Meneja Biashara na Mthamini wa Madini kutoka Tume ya Madini, George Kaseza, akitangaza washindi hao wa ununuzi wa madini ya Almasi, amesema washindi hao kiutaratibu hawapaswi kutangazwa bali watapigiwa simu na kupewa utaratibu, huku alisema zoezi hilo ni endelevu na wanunuzi wajitokeze zaidi

Kwa upande wake Katibu wa Wanunuzi Wadogo wa Madini ya Almasi wilayani Kishapu, Masanja Meja, ameipogeza Serikali kwa kuwajali wazawa kunufaika na Rasilimali za nyumbani, huku wakiomba kwenye ununuzi wa madini hayo ya Mwadui Kodi iondolewe ili wapate kunufaika zaidi.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akiangalia washindi ambao wamekizi vigezo vya kununua madini ya Almasi.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na Kamati ya Siasa Mkoa wa Shinyanga, wakiwa kwenye mnada wa madini ya Almasi ndani ya mgodi wa Mwadui.
Meneja wa mgodi wa madini ya Almasi Mwadui (WDL) Ayoub Mwenda .
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu,Nyabaganga Taraba akizungumza katika mnada huo.

Habari Kubwa