Msaada huo ulikabidhiwa na Katibu Mkuu wa shirika hilo, Felician Mtahengerwa ambaye aliambatana na Mwenyekiti wa Red Cross mkoa wa Manyara Wakili Moses Basila. Ambapo kila kaya imekabidhiwa fedha za kujikimu.
Katika msaada huo, kila kaya imepata kiasi cha 70,000 ambapo zoezi hilo liliongozwa na Mkurugenzi wa Maendeleo na miradi ya shirika hilo, Reginald Mhango pamoja na wafanyakazi wa TRCS na IFRC ambao pia wamefadhili msaada huo wakiwakilishwa na Ndugu Surge Moyo kutoka IFRC
Kufuatia msaada huo, Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Dk. Suleiman Serera ameipongeza TRCS kwa kazi nzuri wanazofanya za kusaidia jamii na kuwakaribisha wilayani humo kwa ushirikiano zaidi hasa kuisaidia wilaya hiyo katika kutokomeza ukame.
Zoezi la kugawa msaada huo lilianza Aprili 27 mwaka huu.