Red Cross yaunga mkono serikali uhamasishaji kufanya usafi

06Dec 2021
Yasmine Protace
Nipashe
Red Cross yaunga mkono serikali uhamasishaji kufanya usafi

TANZANIA Red Cross Society yaungana na serikali katika juhudi za kuhamasisha jamii kufanya usafi wa mazingira katika maeneo yanayowazunguka.

Mbali na kuiunga mkono serikali katika kuhamasisha jamii kufanya usafi,pia nao kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wamefanya usafi katika maeneo ya masoko, shule na hospitali katika Jiji la Dar es Salaam katika maadhimisho ya Siku ya Kujitolea Dunia ambapo kilele chake huwa ni Desemba 5 kila mwaka.

Katika maadhimisho hayo Red Cross Society iliongozwa na Makamu wake wa Rais, Lucia Pande.

"Siku ya kujitolea duniani kila mwaka uadhimishwa ifikapo Desemba 5 kila mwaka," amesema.

Ameongeza kuwa malengo ni kuwakumbusha wana jamii kuona umuhimu wa kujitolea katika maeneo yao kwa kuisaidia jamii inayo wazunguka kufanya usafi wa mazingira.

Amesema  Tanzania Red Cross Society kama taasisi inayoongozwa na kanuni saba ikiwemo kujitolea imeungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha siku hiyo kwa kufanya usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali pia ikiwa ni juhudi za kuunga mkono serikali katika kuhamasisha usafi wa mazingira.

Habari Kubwa