Ripoti unyanyasaji 'House Girls' wa Tanzania Oman yazuiwa

14Nov 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Ripoti unyanyasaji 'House Girls' wa Tanzania Oman yazuiwa

Maofisa waliojitambulisha ni kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi Tenklojia (Costech) wamezuia kuzinduliwa kwa ripoti ya unyanyasaji wa watumishi wa ndani wa kitanzania nchini Oman na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Ripoti hiyo inatokana na utafiti uliofanywa na Shirika la Kimataifa la Kutetea Haki za Binadamu (Human Right Watch) ulitakiwa kuzinduliwa saa nne asubuhi leo Jumanne, katika ukumbi wa Holiday Inn, hata hivyo kabla ya kuzuiwa ripoti hiyo ilikuwa imeshasambazwa kwa waandishi wa habari.

Mmoja wa maofisa hao, Willium Kindeketa amesema wamelazimika kuizuia ripoti hiyo kwa sababu watafiti hawakufuata taratibu zinazotakiwa.

“Kwetu sisi utafiti wowote ule unaofanyika uwe wa kijamii au kisayansi Costech ndio wenye mamlaka ya kupitisha hizo tafiti,” amesema.

Ripoti hiyo ambayo ambayo tayari ishasambaa ilieleza watumishi wa Kitanzania wanaofanya kazi Oman na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) wanakabiliwa na saa nyingi za kazi, kutolipwa mishahara, ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa kimwili kinyume na haki za binadamu.

Habari Kubwa