Ripoti ya CAG yatua Bungeni leo

08Apr 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Ripoti ya CAG yatua Bungeni leo

RIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), imewasilishwa bungeni leo Alhamisi Aprili 8, 2021.

Spika wa Bunge, Job Ndugai, amesema ataikabidhi ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa kamati mbili za Bunge.

Amezitaja kamati hizo kuwa ni Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (Laac).

Ameeleza hayo bungeni muda mfupi baada ya Serikali kuwasilisha taarifa za ukaguzi wa hesabu za wizara, taasisi na mashirika yaliyo chini yao.

Waliowasilisha taarifa ni Wizara ya Tamisemi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Ujenzi na Ofisi ya Rais Utumishi.

Habari Kubwa