Risasi,mabomu yatawala katika hotel ya kifahari Kenya

15Jan 2019
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Risasi,mabomu yatawala katika hotel ya kifahari Kenya

Watu kadhaa wamejeruhiwa na kufuatia mlipuko na milio ya risasi iliyotokea katika eneo la 14 Riverside, Nairobi nchini Kenya ambapo maafisa wa shirika la msalaba mwekundu wamefika eneo la tukio na kufanya huduma ya kwanza.

Mkuu wa polisi wa uchunguzi wa jinai Bw. George Kinoti ni miongoni mwa maafisa wakuu wa polisi waliofika kuratibu operesheni ya kuokoa watu waliokwama ndani ambapo amekiri kuwa bado uchunguzi unaendelea na hawajabaini wahalifu.

Eneo hilo lenye hoteli ya kifahari na ofisi za kampuni mbalimbali, baadhi ya watu waliokwama kwenye vyumba vya jumba hilo wamekuwa wakiandika ujumbe kwenye mitandao wa kijamii wakieleza kwamba wamekwama na kueleza mahali walipojificha ili kupata msaada.

Milipuko miwili mikubwa ilisikika na baadaye ufyatuaji wa risasi, ambapo tayari baadhi ya majeruhi amesafirishwa kupelekwa hospitali.

risasi

Habari Kubwa