Rotary yatoa msaada kwa wazee Moshi

19Oct 2020
Godfrey Mushi
Moshi
Nipashe
Rotary yatoa msaada kwa wazee Moshi

RAIS wa Rotary Club ya Mwika iliyopo Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Esther Towo, amesema tatizo la kipato linalowakabili wananchi wengi hivi sasa na kuwafanya washindwe kufuata utamaduni wa kitanzania wa kusaidia wazee wasiojiweza, umewasukuma kuanzisha mradi wa wazee-

-unaoangalia mahitaji yao muhimu.

Towo amesema suala la kuwatunza wazee sio la serikali peke yake, kwa kuwa mila za kitanzania zinafunza watu wa rika zote kusaidiana, hivyo jamii inapaswa kujenga utaratibu wa kusaidia mahitaji ya wazee wasiojiweza ili kuchuma baraka kwa familia zao.

Kwa nyakati tofauti Towo amezungumza katika Msikiti wa Masjid Nuru uliopo Njia Panda ya Himo, Chuo cha Biblia Mwika na Shokoni, wakati wa zoezi la ugawaji wa magodoro, mito, foronya, shuka na blanketi kwa wazee 12 katika kila eneo.

“Kazi kubwa ya Rotary ni kusaidia jamii ile ambayo wana mahitaji sawa, hatuendi kwa mtu mwenye nacho, tunaangalia wale wenye mahitaji na pia kusaidia jamii ambayo ina shida fulani ili tuwatoe katika hatua moja tuwapeleke hatua nyingine" amesema Towo.

Habari Kubwa