RTO Kotecha awataka waendesha pikipiki kutii sheria za barabarani

07Dec 2021
Neema Emmanuel
Mwanza
Nipashe
RTO Kotecha awataka waendesha pikipiki kutii sheria za barabarani

​​​​​​​KAMANDA wa Usalama barabarani Mkoa wa Mwanza (RTO) Joyce Kotecha, amewataka waendesha pikipiki mkoani humo kufanya kazi kwa kuzingatia na kutii sheria za usalama barabarani ili kudhibiti ajali zinazoepukika.

KAMANDA wa Usalama barabarani Mkoa wa Mwanza (RTO) Joyce Kotecha.

Kamanda Kotecha amesema hayo wakati akizungumza kwenye halfa ya kuwaapisha viongozi wa Chama cha waendesha pikipiki (UWP) mkoani humo.

Kotecha amesema Rais Samia Suluhu Hassan anawapenda sana waendesha bodaboda lakini anawataka wazingatie sheria pamoja na kuwafanyia punguzo la faini lakini wametakiwa kuzingatia sheria ili kupunguza ajali kwa kiasi kikubwa.

Amesema jukumu la viongozi wa UWP ni kuhakikisha wananchi na madereva wanavaa kofia ngumu na wanazingatia sheria za usalama barabarani ili kuokoa maisha ya wananchi.

Aidha, amesema bodaboda anapaswa kumuelimisha abiria asiye vaa kofia ngumu avae na asiye tayari asibembwe, pia Mkoa wa Mwanza mwakani unatarajia kuwa wenyeji wa maadhimisho ya usalama barabarani kitaifa hivyo ni vizuri kufikia siku hiyo tukutwe ajali ni chache na watu wote wapo hai na tuna tii sheria za barabarani.

Habari Kubwa