Ruzuku sio kigezo chama cha siasa kushika dola

01Jul 2020
Dotto Lameck
Dar es Salaam
Nipashe
Ruzuku sio kigezo chama cha siasa kushika dola

NAIBU Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Mohamed Ahmed, amesisitiza kuwa ruzuku sio kigezo kwa chama cha siasa kuwa na nguvu ya kushika dola.

Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Mohamed Ahmed.

Aidha, amevitaka vyama vya siasa kujenga hoja na ushawishi kwa wananchi katika kipindi cha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu

Ahmed amesema katika kuelekea uchaguzi mkuu, vyama vyote vya siasa nchini vinatakiwa vijitazame na kujikosoa kwa hoja zao zilizo imara zenye uwezo wa kuwashawishi wanachama na wananchi kwa ujumla badala ya kutazama ruzuku kwani mfumo wa vyama vingi nchini ulipoanza hakukuwa na uwezo wa kufedha.

Msajili huyo ameongeza kwa kusema vyama vyote vyenye usajili wa kudumu vina haki sawa kwa mujibu wa sheria, na hii kutokana na baadhi ya vyama vyenye uwezo wa ruzuku vimejikuta katika migogoro ya mara kwa mara ambayo imepelekea kuathiri dhana ya msingi mkuu wa vyama vya siasa ambayo ni kushika hatamu ya uongozi na kuongoza dola.

 

Habari Kubwa