Sababu kibano makandarasi Dar

24Oct 2019
Beatrice Moses
Dar es Salaam
Nipashe
Sababu kibano makandarasi Dar

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amewapa siku tano makandarasi wanaosuasua kwenye miradi ya ujenzi wa miundombinu, na kuwa atawakamata na kuvunja mikataba yao.

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, picha mtandao

Makonda aliyasema hayo kutokana na hali ya kusuasua kwa baadhi ya makandarasi waliopo kwenye Mkoa wa Dar es Salaam kutokana na nyaraka za uongo walizoziwasilisha wakati walipoomba zabuni ya miradi waliyokabidhiwa ambayo ipo inayotimiza miezi mitatu lakini bado haijaanza kutekelezwa.

Uongo uliouonyesha kwenye maombi kupitia nyaraka ulizojaza pesa walizoonyesha wewe ni ‘class one’, una pesa za kutosha, una vifaa vya kutosha na baadhi ya makandarasi nimebaini hata vifaa hawana hata hizo fedha walizozionyesha kwenye makaratasi hawana fedha wala vifaa.

Alisema baadhi ya makandarasi hao wamekuwa wakizungusha fedha za ‘[mobilization’ kwenye miradi mingine kwa kuwa hawana fedha, hivyo wamekuwa wakikwamisha kukamilisha kwa miradi tofauti na muda uliopangwa.

Alizionya bodi zote katika Mkoa wa Dar es Salaam zinazotoa zabuni kwa makandarasi wasio na uwezo nao watashughulikiwa ikiwamo kufukuzwa kazi.

Aliitaja baadhi ya miradi hiyo ni ujenzi wa barabara ya Kivule, Buguruni Kisiwani, Mto Ng’ombe na barabara ya Kawe.

“Mnafahamu uwezo wangu na sina kigugumizi kwenye hatua, makandarasi wanafanya mchezo kwa sababu aidha walipata kazi kwa kuhonga na waliowahonga wanashindwa kuwasimamia.

Alisema alishawaeleza makandarasi wenye changamoto ya malipo ofisi yake na ya Katibu Tawala wa Mkoa ipo wazi wafike ili wasaidiwe kukamilishiwa malipo yao, lakini kumekuwa na ukimya.

Makonda alibainisha atashughulika na makandarasi wote wanaotekeleza miradi katika mkoa wake, hata kama waliingia mikataba na wizara mradi miradi hiyo inahusu mkoa wa Dar es Salaam, atatumia mamlaka aliyonayo kuwabana ipasavyo.

Makonda ameitangaza hatua hiyo ukiwa ni mwezi tangu Rais Johm Magufuli aliposema kuwa haridhishwi na kasi ya utekelezaji miradi Dar es Salaam, hasa miradi ya machinjio ya Vingunguti na ufukwe wa Coco, na kuhoji kama mkoa huo una viongozi.

Habari Kubwa