Sababu wanafunzi kujiua baada ya matokeo kutoka zatajwa

26Jan 2022
Mary Kadoke
DAR ES SALAAM
Nipashe
Sababu wanafunzi kujiua baada ya matokeo kutoka zatajwa

WADAU wa elimu nchini wameanisha kuwa matarajio makubwa ya jamii, wazazi na mtaala kuwa ni chanzo cha matukio ya wanafunzi kujiua baada ya kufeli mitihani yao ya mwisho au kupata matokeo kinyume na malengo yao.

Akiainisha njia za kupambana na suala hilo, mshauri kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Enea Muhando amesema ujuzi wa kupambanua changamoto za kimaisha itasaidia kupambana na wimbi hili.

“Siku zote swali langu huwa, mwanafunzi anafeli nini na anafaulu nini. Anayefaulu, anafaulu pia maisha baada ya shule? Elimu hii itamsaidia kupambana na presha inayotokana na kufeli mtihani,” amesema Muhando.

Katibu wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT),Wilaya ya Kinondoni,Evod Kanyaiyangiro, ameelekeza lawama zake kwa wazazi wenye matarajio makubwa ya ufaulu kwa wanafunzi baada ya kuwekeza pesa nyingi kwao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la HakiElimu Dk.John Kalage amesema kujiua kwa wanafunzi kunatokana na matarajio makubwa ya ufaulu kutoka kwa mwanafunzi mwenyewe, walimu pamoja na wazazi.

Dk. Idephonce Mkama kutoka Chuo Kikuu cha Arch, Bishop Mihayo kilichopo Tabora amehimiza walimu kuwaandaa wanafunzi kisaikolojia kabla na baada ya mitihani ili maamuzi yao ya mwisho wanapokupambana na changamoto yawe kutafuta mbadala badala ya kujinyonga.

Katika hali isiyo ya kawaida, Mkuu wa wilaya ya Butiama Moses Kaegele alitangaza tukio la kujinyonga kwa mwanafunzi wa kidato cha nne aliyefikia maamuzi hayo baada ya kupata daraja la pilina si  la kwanza.

Habari Kubwa