Sababu ya rafiki wa Lowassa, Khamis Mgeja iliyomrudisha CCM 

06Mar 2019
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Sababu ya rafiki wa Lowassa, Khamis Mgeja iliyomrudisha CCM 

Mwanasiasa mkongwe na maarufu nchini ambaye aliyekuwa Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Khamis Mgeja ametangaza kuachana na chama hicho na kujiunga Chama cha Mapinduzi (CCM).

Khamis Mgeja akizungumza na waandishi wa habari juu ya uamuzi wake wa kurudi ccm.

Mgeja ametangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo Jumatano Machi 6, na kusema amejitathimini kwa kina na kwa upana na kuona kwa sasa sababu zilizomfanya kuhamia Chadema hazipo.

Amesema amerudi CCM kutokana na utendaji wa Rais Dk. Magufuli kuwa mzuri na ndiyo ambao ulikuwa malengo alipokwenda Chadema awali.

"Rais Magufuli amefanya kazi kubwa ikiwa ni pamoja na kuondoa rushwa, ufisadi, kuweka nidhamu ya nchi na chama na nchi kwa sasa inakwenda sawa hakuna sababu ya kubaki Chadema kwanza ni chama ambacho hawashauriki, niliwashauri waendeshe chama kisiasa lakini wamebaki wanaendesha chama kiharakati" Amesema Mgeja.

Mgeja aliyeambatana na familia yake amesema alitengana na familia yake kiitikadi lakini anawaomba radhi na sasa wanakwenda sawa.

 

Habari Kubwa