Salome Kitomari achaguliwa mweka hazina MISA

08Jun 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Salome Kitomari achaguliwa mweka hazina MISA

MWENYEKITI wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA Tan), Salome Kitomari, amechaguliwa kuwa Mweka Hazina wa MISA Kanda.

Salome Kitomari

Kikao cha bodi inayoundwa na wenyeviti wa nchi tisa za Kusini Mwa Afrika (RGC), kilimchagua Salome Kitomari  kuwa mweka hazina , wengine ni Golden Maunganidze (Mwenyekiti MISA Zimbabwe), aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa MISA Kanda ,na Nkoale Ts’oana Joseph (Mwenyekiti MISA Lesotho) aliyechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti.

Katiba za MISA kwenye nchi hizo zina mjumbe wa bodi mwenye taaluma ya fedha, ambaye atakuwa na wajibu wa kumsaidia Mwenyekuti wake kuhakikisha mambo ya fedha za jumla yanakwenda vizuri.

Aidha, Wenyeviti hao waliamua kwa pamoja kuhamishia Makao Makuu nchini Zimbabwe, kutoka Zambia ambao waliongoza tangu mwaka 2018.

Akizungumza mara baada ya uchaguzi huo, Mwenyekiti Mpya alisema “Hii ni fursa nzuri kwa MISA kufafanua na kutengeneza mikakati tuliyojiwekea ambayo itaimarisha msimamo wa uongozi kikanda juu ya uhuru wa kujieleza na upatikanaji wa taarifa.”

MISA ilianzishwa mwaka 1996 na inaundwa na nchi za Tanzania, Malawi, Zambia, Msumbuji, Lesotho, Botswana, Zimbabwe, Eswatin, Namibia, Afrika Kusini na Angola ikiwa ni kati ya nchi 16 za SADC, na jukumu lake kuu ni uhuru wa kujieleza na upatikanaji wa taarifa.

Habari Kubwa