Salum Mwalimu: Maalim Seif angeamia CCM ingeleta taharuki

20Mar 2019
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Salum Mwalimu: Maalim Seif angeamia CCM ingeleta taharuki

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)  kimesema Maalim Seif Shariff  Hamad angehamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ingeleta taharuki na mshangao mkubwa sana.

Maalim Seif Shariff  Hamad

Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu, wakati akizungumza waandishi wa habari  na kusema Chadema inaamini alichokifanya Maalim Seif kimelenga maslahi mapana ya mabadiliko katika nchi Tanzania Bara na Visiwani kuliko maslahi yake binafsi wala chama chochote.

Aidha Mwalimu amesema kuwa wamekubaliana wakati Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ikijadiliwa, wabunge hao wasimame kutetea hilo.

Amesema kuwa kikao cha Sekretarieti kilichokaa kimependekeza wabunge wake wafanye mambo mawili bungeni likiwemo kusimama kidete kutetea haki na maslahi ya askari magereza na watu waliopo gerezani.

Pia amesema kupitia  Kamati ndogo za sheria wazipitie sheria zinazoweza kubadilishwa ambazo zinasababisha  kundi hilo kukosa haki kwa wakati.

"Wiki iliyopita Mwenyekiti wa Taifa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini,  walieleza maisha ya Magereza hasa Segerea alikokaa siku 104," Amesema Mwalimu