Samia aagiza maiti kutozuiwa hospitalini

08Jun 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Samia aagiza maiti kutozuiwa hospitalini

Rais Samia Suluhu Hassan, amemuelekeza Waziri wa Afya, Dk Dorothy Gwajima kuweka mpango mzuri wa ndugu kulipa deni la hospitali ili ikitokea mgonjwa wao amefariki dunia wakati akitibiwa maiti isizuiwe.

“Haileti maana mtu amefiwa anawaza msiba, kusafirisha na kuzika halafu bado unazuia maiti, hili haliwezekani.Nakuelekeza Waziri hebu nendeni mkaweke mpango mzuri wa kulipa deni na sio kuzuia maiti,” amesema.

Ametoa kauli hiyo leo Jumanne Juni 8, 2021 katika mkutano wake na wanawake wa Dodoma.

Amesema siyo sawa maiti kuzuiwa na kwamba ni muhimu ukawekwa utaratibu wa kulipa deni la matibabu wakati taratibu za msiba zikiendelea.

“Wananchi muelewe sio kwamba deni lisilipwe bali uwekwe mpango mzuri na mmoja wapo ni kulipa wakati matibabu yakiendelea na muhimu zaidi ni kuwa na bima ya afya,” amesema Samia.

Habari Kubwa