Samia ataka viongozi kukiri makosa

08May 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Samia ataka viongozi kukiri makosa

RAIS Samia Suluhu amesema moja ya mafunzo makubwa katika kitabu kilichozinduliwa leo cha maisha ya Rais wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Ally Hassan Mwinyi ni umuhimu kwa viongozi kukiri makosa pale wanapokosea.

Amesema viongozi  ni muhimu kukubali kukiri pale wanapokosea ili kutafuta  suluhisho  la makosa  yao kwa kuwa kukosea ni sehemu ya maisha ya binadamu.

“Viongozi siyo malaika viongozi ni binadamu na binadamu kwa kawaida ameumbiwa kufanya makosa Mzee Mwinyi  anakiri katika kipindi chake cha uongozi yalifanyika baadhi ya makosa”-Rais Samia Suluhu.

Kitabu hicho kilichozinduliwa leo katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere  JNICC kimeelezwa kuwa na maneno yapatayo  139,307 kilichchapishwa na Mkuki na Nyota na kwamba kimejibu maswali mengi yanayomhusu Mzee Mwinyi.

 

Habari Kubwa