Sampuli 5,106 zapimwa DNA kanda ya kati

11Dec 2019
Augusta Njoji
Dodoma
Nipashe
Sampuli 5,106 zapimwa DNA kanda ya kati

MAMLAKA ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), kanda ya kati imepokea sampuli 36 za kupima vinasaba (DNA), huku asilimia 90 ya sampuli zililenga kuangalia uhalali wa wa baba wa mtoto.

Hayo yamebainishwa leo mkoani Dodoma na meneja wa kanda hiyo, Musa Kuzumila wakati akitoa ripoti ya chunguzi zilizofanyika ndani ya miaka miwili na nusu tangu kuanzishwa kwa ofisi hiyo.

Amesema majibu ya sampuli hizo yatasaidia kumaliza kesi au migogoro kwa wakati.

"Katika kipindi cha miaka miwili na nusu tumekusanya sampuli 5,106 ambazo zimeenda kufanyiwa uchunguzi katika maabara zetu na sampuli hizi ni pamoja na madawa ya kulevya, DNA na kuangalia sumu," amesema Kuzumila.

Katika hatua nyingine, amesema ifikapo 2028 serikali itapiga marufuku matumizi ya kemikali ya zebaki.

Habari Kubwa