Scania Tanzania yakarabati madarasa shule ya msingi Vingunguti

31Mar 2019
Gwamaka Alipipi
Dar es salaam
Nipashe Jumapili
Scania Tanzania yakarabati madarasa shule ya msingi Vingunguti

SHIRIKA la Scania Tanzania limefanya ukarabati wa madarasa mawili katika Shule ya Msingi Vingunguti jijini Dar es Salaam, ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha miundombinu ya shule, kuongeza ufaulu, pamoja kuboresha mazingira ya kusomea kwa wanafunzi.

Naibu Meya wa Manispaa ya Iala, Omary Kumbilamoto ( kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Shirika la Scania Tanzania, Merek Rucinski wakikata utepe kufungua madarasa yaliyokarabatiwa na shirika hilo.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi madara hayo, Mkurugenzi wa Shirika la Scania Tanzania, Marek Rucinski alisema wataendelea kuisaidia shule hiyo kwa muda wa miaka mitatu.

“Ukiisaidia shule utawapa hamasa walimu na wanafunzi kufanikisha malengo yao, kwa Shirika la Scania kufanya vitu kama hivi ni kawaida, tunaweza kuboresha mfumo wa usafiri bila ya kuharibu mazingira.. lakini furaha yetu ni kuona wanafunzi wakisoma sehemu nzuri,” alisema Rucinski.

Naye Mwalimu Mkuu msaidizi wa shule hiyo, Neema Sungura alisema shule ya msingi Vingunguti ilianzishwa mwaka 1974, kwa sasa ina wanafunzi 2227 na walimu 33, vyumba vya madarasa 16 wakati mahitaji halisi ni 21.

Alisema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo, upungufu wa madara, uchakavu wa vyoo, upungufu wa vitabu, ukosefu wa vifaa vya kufanyia usafi,upungufu wa samani, kujaa maji wakati wa mvua, ukosefu wa ziara za mafunzo kwa wanafunzi.

Habari Kubwa