Maeneo mengine yaliyolalamikiwa ni Mahakama, Polisi, Ardhi na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
Hayo yalielezwa jana jijini Dar es Salaam na Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni, Elizabeth Mokiwa wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu yao kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu.
Mokiwa alisema katika kipindi hicho kesi 162 zilipokelewa wakilalamikia vitendo vya rushwa katika taasisi hizo.
Mokiwa alisema katika kesi hizo malalamiko kwa sekta binafsi yaliyopokelewa yalikuwa 68, TAMISEMI 24, Ardhi 15, Polisi 13, Mahakama 13, TBS 11 na malalamiko 16 yalihusu mtu mmoja mmoja.
Aidha, alisema katika kipindi hicho wamefuatilia miradi yenye thamani ya Sh. bilioni 11 kwa lengo la kuhakikisha kuwa fedha zinazotolewa zinatumika kwa usahihi kwa kuzingatia ubora, thamani ya fedha na muda uliopangwa.
Hivyo, Mokiwa aliwataka wananchi wa Kinondoni na Ubungo kutumia vizuri siku za kusikiliza malalamiko na kero zilizotengwa na taasisi hiyo, lengo likiwa ni kuhakikisha vitendo vya rushwa vinatokomezwa.
Aidha, Mokiwa alisema katika kufanikisha mikakati yake TAKUKURU imejipanga kushirikiana na Chama cha Skauti chini ya Mpango wa TAKUSKA kwa kutoa elimu ya mapambano dhidi ya rushwa ikiwamo umuhimu wa ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo.