Mollel amesema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo amesema kuwa hawakuamini walipopata taarifa za awali lakini baada ya aliyekuwa Makamu wa Rais Samia Suluhu kutangaza ndipo wakaamini kuwa ni kweli.
“Kifo cha Hayati Rais Dk. Magufuli kimetugusa sana wafanyabiashara wa madini jitihada na maono yake yalipandisha makusanyo ya tozo za madini kutoka millioni 160 kwa mwaka hadi kufikia billioni 2,”Amesema Mollel.
Aidha, Mollel amesema wameona juhudi zake binafsi za kujengwa kwa ukuta Mererani ambapo mpaka sasa wameona faida kubwa za ukuta huo ikiwemo kulinda usalama wao wanapokuwa kazini tofauti na awali, uzalishaji kuongezeka pamoja tozo za serikali kukusaywa kwa kiasi kikubwa.
“Ameifanikisha sana sekta ya madini kwa kuelekeza masoko ya madini yajengwe kila Mkoa wenye shughuli za uchimbaji madini, tulimweleza kero zetu kuhisiana tozo sumbufu, alizipokea na kutoa maelekezo kwa Bunge kurekebisha ambayo ilikuwa ni tozo ya ongezeko la thamani, VAT na tozo ya zuio na kushuka kutoka asilimia 18 hadi kufikia asilimia 5,” Amesema Mollel.