SENAPA yakamata ng'ombe 8,000

12Jan 2018
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
SENAPA yakamata ng'ombe 8,000

Askari wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti SENAPA wamefanikiwa kukamata zaidi ya Ng'ombe 8,000 ambao wanadaiwa kuingizwa katika hifadhi hiyo kutoka katika baadhi ya vijiji wilaya za Serengeti, Bunda, Bariadi, Tarime na Meatu ikiwa ni kinyume cha sheria.

Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, William Mwakilema, amewaambia wajumbe wa kikao cha kawada cha kamati ya ushauri ya mkoa wa Mara kuwa idadi hiyo kubwa ya mifugo imekamatwa ikingizwa kuchunga katika hifadhi hiyo nyakati za usiku ikitokea katika baadhi ya vijiji hivyo vinavyozunguka hifadhi hiyo.

Mwakilema, amesema kuwa tatizo hilo la uingizaji wa mifungo katika eneo hilo ambalo limehifadhiwa linaendelea kuonge zeka kila kukicha hatua ambayo inaweza kusababisha kuibuka kwa magonjwa kutoka kwa wanyama pori kwenda kwa mifugo au kutoka kwa mifugo inayofugwa kwenda kwa wanyama pori.

Mkuu wa mkoa wa Mara, Adam Malima, ameagiza viongozi wa Serikali za vijiji hadi wilaya kuchukua hatua za kuzuia uingizaji wa mifugo katika hifadhi hiyo, huku Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini, Esther Matiko, akishauri maafisa mifugo kuelimisha wafugaji kuanza kufuga kisasa ili kuepuka adha hiyo.

Habari Kubwa