Serikali kuipa nguvu sekta binafsi ya viwanda

23May 2020
Neema Emmanuel
MWANZA
Nipashe
Serikali kuipa nguvu sekta binafsi ya viwanda

Serikali imepanga kuipa nguvu sekta binafsi ya viwanda nchini ili viweze kujiendesha kwa kufanya uzalishaji wenye tija utakaoviwezesha kulipa kodi na tozo mbalimbali za serikali na kuchangia uchumi wa nchi.

Hayo yamesemwa Jijini Mwanza na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya, wakati alipotembelea Kiwanda cha kuchakata Minofu ya Samaki aina ya Sangara cha Tanzania Fish Processors Limited.

Amesema awamu hii vimezaliwa viwanda vingi vikubwa na vidogo hivyo sekta binafsi wachukue nafasi ya kujitangaza ili kuongeza masoko.

 “Viwanda vya zamani kweli vimekufa lakini vimezaliwa vingine kama ilivyo kwa binadamu mwengine anakufa mwengine anazaliwa ata teknolojia uwezi kutegemea ile ya zamani kwa sababu mpya nazo zinaingia”amesema Manyanya

 Amelitaka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kuzingatia matumizi ya lugha ya kiswahili na kuhakikisha bidhaa zote zinazotoka Tanzania kwenda nje ya nchi zikuwa na alama inayoeleza kwa lugha hiyo.

Kwa upande wake Meneja Rasilimali watu kutoka  kiwanda cha Tanzania Fish Processors Limited, Godfrey Samweli, amesema changamoto zinazowakabili kwa sasa ni ufinyu wa chumba cha baridi kutoweza kuhimili mzigo unapokuwa mkubwa hivyo ameiomba Serikali kuongeza ukubwa wa chumba cha baridi cha kuifadhia samaki katika uwanja wa ndege wa kimataifa Mwanza “Cold room” ili kusaidia kuhifadhi mzigo n`ikatayosaidia kuhifadhi mzigo mkubwa zaidi kabla ya kupakizwa kwenda nje ya nchi .

 “Wiki ijayo tuna mpango wa kusafirisha tani 25 lakini tulipoenda kuangalia chumba cha baridi hakina uwezo wa kubeba tani hizo”amesema Samweli

Habari Kubwa