Serikali kuajiri 500 Uhamiaji

07Aug 2019
Romana Mallya
DAR ES SALAAM
Nipashe
Serikali kuajiri 500 Uhamiaji

SERIKALI imesema imebaini upungufu wa askari katika Idara ya Uhamiaji hasa maeneo ya viwanja vya ndege na tayari imetangaza nafasi za ajira ili kutatua changamoto hiyo.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, aliyasema hayo jana muda mfupi baada ya kumaliza ziara yake kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume visiwani Zanzibar.Alisema katika bajeti ya mwaka huu wa fedha, serikali imepanga kuajiri jumla ya askari 500 ambao watakwenda kufanya kazi kwenye viwanja vya ndege mbalimbali nchini.Alisema Idara ya Uhamiaji hivi karibuni ilitangaza nafasi za kazi 200 ambazo ni kati hizo 500 zinazotakiwa kutolewa kwa mwaka huu wa fedha."Tuna changamoto ya watendaji katika viwanja vyetu vya ndege, hii inatokana na uhakiki ambao serikali iliufanya na kubaini wapo watu walioajiriwa pasipo kufuata taratibu na wengine wakilipwa mishahara hewa, baada ya kuondolewa kumekuwa na upungufu.“Hivi karibuni, Idara ya Uhamiaji ilitangaza nafasi za ajira na tutahakikisha viwanja vyote vya ndege nchini vinapata watendaji wapya," Masauni alisema.Aliwataka wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama katika uwanja huo kufanya kazi kwa ushirikiano ili yale yaliyotokea viwanja wa ndege vya Mwanza na Kilimanjaro, yasitokee tena.“Kama mtakumbuka yaliyotokea Uwanja wa Ndege wa Mwanza na kule Kilimanjaro, ni aibu kwa taifa na vyombo vilivyopo vya ulinzi na usalama, madini na dhahabu kukamatwa Kenya wakati vyombo hivi vilikuwapo," alisema.Masauni aliongeza kuwa Rais John Magufuli aliwanyooshea kidole polisi kutokana na tukio hilo la aibu. 

 

 

Habari Kubwa