Serikali kuwaibua wabunifu vijijini kutatua changamoto za kilimo

18May 2022
Renatha Msungu
DODOMA
Nipashe
Serikali kuwaibua wabunifu vijijini kutatua changamoto za kilimo

WAZIRI wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Adolf Mkenda amesema serikali inajikita kufika maeneo ya vijijini kuibua wabunifu watakaoleta bunifu zenye tija katika kutatua changamoto za kilimo.

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda akizungumza na waandishi wa habari kwenye wiki ya ubunifu,kulia ni Mkurugenzi wa COSTECH DK Amosi Nungu.

Profesa Mkenda amebainisha hayo jijini Dodoma leo wakati akifungua mdahalo ulioandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia(COSTECH) katika wiki ya ubunifu inayoenda sambamba na mashindano ya Kitaifa ya Sayansi Teknolojia na ubunifu (MAKISATU).

Prof. Mkenda amesema kuna wabunifu mbalimbali wasiojulikana mitaani na pembezoni hivyo jukumu la serikali ni kuwatangaza na kuwaibuawabunifu hao kutoka maeneo ya vijijini ikiwemo maeneo ya shule ili kuwaendeleza.

"Serikali haiwezi kuwatelekeza wabunifu pamoja na bunifu zao,bali inafanya jitihada ya kuendeleza bunifu zinazoibuliwa ili wabunifuwazidi kupanua wigo wa ubunifu,"amesema Prof. Mkenda.

Naye Mkurugenzi wa COSTECH, Dk.Amosi Nungu amesema wiki ya ubunifu ni sehemu muhimu ya kuendelea kuchagiza ubunifu wenye tija katika maendeleo ya nchi kwenye nyanja mbalimbali.

Dk Nungu, amesema pia wiki ya ubunifu inawapa nafasi wabunifu kuendelea kujuana ikiwemo kupanua wigo wa kazi za bunifu wanazofanya kwa kila mmoja kuangalia ujuzi wa mwenzie.

Amefafanua zaidi kuwa COSTECH imebaini ubunifu mwingi uko mtaani na unahitaji kuibuliwa ili uweze kupiga hatua kutoka chini hadikufikia kimataifa.

"COSTECH tumeamua kufanya mdahalo ambao unaonekana moja kwa moja ili wabunifu wengine na Watanzania kwa ujumla kuweza kuonafursa za masuala ya ubunifu,"amesema Dk Nungu.

Habari Kubwa