Serikali kuwasilisha muswada wa bima ya afya bungeni

19Apr 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Serikali kuwasilisha muswada wa bima ya afya bungeni

Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema inatarajia kuwasilisha bungeni muswaada wa bima ya afya kwa wananchi wote hapa nchini mwezi Juni mwaka huu baada ya kukamilisha mchakato wa kupokea maoni mbalimbali kwa wadau wa afya na kuwa na sheria bora.

Naibu Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dk. Godwin Molell, ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu, Janeth Elias, aliyetaka kujua serikali ina mpango gani wa kuwasaidia wajasirimali wadogo kupata bima ya afya kupitia vikundi vya pamoja.

Dk. Molell amesema dhamira ya serikali ni kuhakikisha kila mwananchi anapata matibabu kupitia bima ya afya mpango utakaohusika kila mwananchi baada ya muswaada huo kukamilika baada ya kuwasilishwa bungeni kujadiliwa na wabunge na baadae kuwa sheria baada ya bunge kupitishwa muswaada huo wa bima ya afya kwa kila mwananchi na kuwa sheria.

Naibu waziri huo wa afya amesema mpaka sasa jumla ya vikundi elfu 32, 343 vimesajili kupata huduma ya afya kupitia mfumo wa vifurushi vya bima ya afya mpango ambao unaendele kwa sasa kote nchini.

Wakati huo huo Dk. Molell amesema serikali ina mpango endelevu wa kutoa elimu kwa wananchi wakiwemo wachimbaji wadogo na wakubwa katika migodi juu ya matumizi ya kemikali aina ya zebaki ambayo imekuwa ikisababisha madhara kwa wananchi kutokana na kutokuwa na elimu ya matumizi ya kemikali hizo kwa sasa.

Habari Kubwa