Serikali sasa kula sahani moja na watengeneza feki

02Aug 2017
Renatha Msungu
DODOMA
Nipashe
Serikali sasa kula sahani moja na watengeneza feki

SERIKALI imesema ili kulinda viwanda yake nchini itahakikisha inashughulika na atakaotengeneza bidhaa feki.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji katika ziara yake ya kutembelea watu wanaokopeshwa na Mfuko wa Self mjini Dodoma.

"Serikali itashughulikia changamoto ya bidhaa feki kwa haraka ili kulinda viwanda vya hapa nchini kwasababu mtu anayetengeneza bidhaa feki ni mwizi,"alisema Naibu Waziri huyo

Akizungumzia kuhusu urejeshaji wa mikopo,Dk.Kijaji kutorejeshwa kwa mkopo kwa kiwango kikubwa katika baadhi ya taasisi kinachangiwa na kukosekana kwa tathimini kwa wakopaji juu ya shughuli wanazokwenda kufanya.

Habari Kubwa