Serikali yaagiza kuachiwa wavuvi waliokamatwa Bahari ya Hindi

16Jan 2019
Halima Kambi
DAR ES SALAAM
Nipashe
Serikali yaagiza kuachiwa wavuvi waliokamatwa Bahari ya Hindi

SERIKALI imetoa agizo la kuachiwa kwa wavuvi wote waliokamatwa kwa kosa la kutokuwa na leseni katika wa Pwani wa Bahari ya Hindi. 

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega.

Maagizo hayo yametolewa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega kufuatia na taarifa zilizotolewa katika vyombo vya habari kuwa Wavuvi wa Ukanda huo katika soko la Feri jijini Dar es Salaam kushindwa kwenda kuvua kwa sababu ya kukamatwa kwa kosa la kutokuwa na leseni za uvuvi kwa mwaka huu 2019. 

Naibu Waziri amewataka maafisa  uvuvi wa Wizara na Halmashauri kuwafuata wavuvi katika mialo yao ili kuwakatia leseni kwa wenye sifa kulingana na sheria za uvuvi.

Habari Kubwa