Serikali yanunua mtambo mpya kufyatua vitambulisho vya NIDA

01Apr 2020
Augusta Njoji
DODOMA
Nipashe
Serikali yanunua mtambo mpya kufyatua vitambulisho vya NIDA

 SERIKALI imesema imenunua mashine mpya yenye thamani ya sh bilion 8. 5 kwa ajili ya kufyatua vitambulisho vya NIDA.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Georgre Simbachawene.

Mashine hiyo ina uwezo wa kutoa vitambulisho 9, 000 ambapo kwa saa wanaendelea na zoezi la ufungaji mashine hizo na zoezi la utoaji wa vitambulisho litakamilika ndani ya miaka miwili au zaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma leo Aprili 1,2020 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Georgre Simbachawene amesema hadi sasa ni watu milioni 6 tu ambao tayari wamepata vitambulisho.

Amesema ucheleweshaji wa vitambulisho hivyo umetokana na mashine za awali kutokuwa na ubora kwani zilikiwa chakavu. 

Habari Kubwa