Serikali yaongeza Sh.bilioni 33 kwenye bajeti ya Tarura

15Apr 2019
Augusta Njoji
DODOMA
Nipashe
Serikali yaongeza Sh.bilioni 33 kwenye bajeti ya Tarura

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo, amesema serikali imeongeza Sh. bilioni 33 kwenye bajeti ya Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini(Tarura) kutokana na kilio cha wabunge wengi-

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo.

wakitaka fedha ziongezwe kwa wakala huo ili kutimiza majukumu yake.

Akihitimisha hoja ya makadirio ya bajeti ya Wizara yake kwa mwaka ujao wa fedha leo bungeni, Jafo amesema fungu namba 59 la Ofisi hiyo zimeongezwa fedha hizo ambazo zitapelekwa Tarura kwa ajili ya ujenzi wa barabara.

“Baada ya kusikia kilio cha wabunge humu ndani serikali imeona iongeze Sh.Bilioni 33 ambazo zitakwenda Tarura kutatua matatizo ya wananchi wetu,”amesema.

Ameeleza kuwa bajeti ya maendeleo ya Ofisi hiyo itasomeka Sh.Bilioni 496.5 badala ya Sh.Bilioni 463.5 na hivyo katika miradi ya maendeleo na matumizi ya kawaida itakuwa Sh.Bilioni 550.2. “Bajeti nzima ya Tamisemi itakuwa na Sh.Trilioni 6.24,”amesema.

Habari Kubwa