Serikali yatenga bil. 4 kununua mashine za kuchakata mazao

20Apr 2021
Na Mwandishi Wetu
Dodoma
Nipashe
Serikali yatenga bil. 4 kununua mashine za kuchakata mazao

WIZARA ya Viwanda na Biashara imetenga shilingi bilioni 4 kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kwa ajili ya ununuzi wa mashine ndogo na kisasa za kuzalisha na kuchakata mazao ya wakulima kupitia Shirika la kuhudumia viwanda vidogo nchini (SIDO).

Xaud Kigahe.

Hayo yamesemwa leo April 20, mwaka huu bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa viwanda na biashara, Xaud Kigahe, wakati akijibu swali la Mbunge wa Vunjo Charles Kimei aliyetaka kujua Serikali ina mkakati gani kupitia SIDO katika kutengeneza mashine zitakazosaidia kuchakata mazao ya wakulima ambao mazao yao yamekuwa yakiharibikia shambani na sokoni kwa kukosekana kwa viwanda vya kuchakata mazao hayo.Kigahe amesema mpango huo utakwenda sawia na utoaji wa elimu kwa wajasiriamali wadogo kuhusiana na namna ya kutambua umuhimu wa mashine hizo wakati wa kuzitumia na kuwa na tija kwao kwa kuwapatia mapato baada ya kuchakata mazao yao kupitia mashine hizo zitakazokuwa zinatengenezwa SIDO kote nchini.

Habari Kubwa