Serikali yazindua boti ya kubeba wagonjwa

29Jul 2021
Na Mwandishi Wetu
Lindi
Nipashe
Serikali yazindua boti ya kubeba wagonjwa

SERIKALI kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) imeleta neema kwa wakazi wa Kilwa Kisiwani na Lindi Kitunda baada ya kuwapelekea boti mbili mpya kwa ajili ya kubeba abiria (Passenger Fibre Glass Boat) na nyingine kwa ajili ya kubeba wagonjwa (Ambulance Fibre Boat), zilizojengwa na kampuni-

-za kizalendo kutoka Tanzania za Songoro Marine Transport Boatyard ya jijini Mwanza na kampuni ya Sam & Anzai Boat Builders Co. Ltd ya Dar Es Salaam.

Boti hizo mbili ambazo ni MV. Lindi itakayokuwa inatoa huduma ya kubeba abiria kati ya Lindi na Kitunda na MV. Lukila itakayokuwa inatoa huduma ya kubeba wagonjwa katika eneo la Kilwa Kisiwani zimekabidhiwa rasmi katika hafla fupi iliyofanyika katika eneo la feri mkoani Lindi ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa huo Zainab Telack.

“Ninafurahi kusikia kuwa ununuzi wa boti hizi umefanyika kupitia bajeti ya Serikali kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 99 kwa boti ya abiria na shilingi 217,600,000.00 kwa boti ya kubeba wagonjwa fedha yote ikiwa imetolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania’’ amesema Zainab Telack.