SGR yaisababishia hasara serikali Bil. 35.6/-

08Apr 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
SGR yaisababishia hasara serikali Bil. 35.6/-

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere, imebaini kuwa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), umeisababishia serikali hasara ya kiasi cha Bil. 35.6/- kutokana na kuajiri wafanyakazi wa kigeni.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Kichere amesema hasara hiyo inatokana na uwepo wa wafanyakazi wa nje na wasiokuwa na vibali vya kufanya kazi wapatao 1, 538.

“Ujenzi wa reli ya kisasa SGR ina wafanyakazi wengio wa kigeni wasio na vibali vya kufanya kazi wapatao 1, 538 walioajiriwa bila vibali hilo limesababishia hasara serikali ya Bilioni 35.6,” amesema Kichere.

Mapema leo ripoti hiyo iliwasilishwa bungeni kwa ajili ya wabunge kuanza kuijadili.

Habari Kubwa