Shamimu na mumewe kuhukumiwa Jumatano

28Mar 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe Jumapili
Shamimu na mumewe kuhukumiwa Jumatano

MAHAKAMA Kuu kitengo cha Uhujumu Uchumi na Makosa ya Rushwa, maarufu kama Mahakama ya Mafisadi iliyopo Jijini Dar es Salaam, imepanga kutoa hukumu dhidi ya mfanyabiashara, Abdul Nsembo (45) maarufu kama Abdulkandida na mkewe, Shamim Mwasha (41) Jumatano Machi 31, Mwaka huu.

Hukumu hiyo itatolewa baada ya upande wa mashtaka na wa utetezi kumaliza kutoa ushahidi wao.

Upande wa mashtaka ulipeleka mashahidi sita na vielelezo NANE huku upande wa utetezi ulikuwa na mashahidi watatu.

Shamimu ambaye ni mmiliki wa Blog ya 8020 na mumewe Nsembo, wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroini gramu 439.70, wanadaiwa kutenda tukio hilo Mei mosi 2019 huko Mbezi Beach jijini Dar es Salaam. Kesi hiyo inasikilizwa na Jaji Elinaza Luvanda.

Habari Kubwa