Shekh Mkuu Katavi: Waislamu swala ya Eid mfuate maelekezo ya serikali

21May 2020
Neema Hussein
Katavi
Nipashe
Shekh Mkuu Katavi: Waislamu swala ya Eid mfuate maelekezo ya serikali

​​​​​​​SHEKH Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mashaka Kakulukulu, amewataka waislam wa Mkoa huo kuswali swala ya Eid kwa kufata maelekezo ya serikali ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona ikiwemo kuzingatia kuachiana mita moja kwa kila mtu na swala hiyo haitoswaliwa katika-

Shekh Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mashaka Kakulukulu, akiongea na wandishi wa habari ofisi kwake namna swala ya Eid itakavyoswaliwa kutokana na hili janga la ugonjwa wa Corona.

-viwanja vya wazi kama ilivyokuwa ikiswaliwa miaka iliyopita.

Kakulukulu amesema hayo jana wakati akizungumza na wandishi wa habari ofisi kwake na kusema kuwa kuanzia siku ya ijumaa misikiti yote ya Mkoa huo wameielekeza kutoa shukurani kwa Mungu kwa kuswali lakaa mbili za shukurani na kutoa sadaka kwa yatima, wajane, na wasiojiweza wakiunganisha na dhakatul fitiri kwa ajili ya kulipinga janga hilo.

Amesema wanamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kupunguza idadi ya wagonjwa, basi kwa kufanya hivyo anaamini Mwenyezi Mungu ataliondosha kabisaa janga la corona.

Aidha, Kakulukulu amesema endapo itatokea msikiti kujaa basi waumini hao wasilazimishe kuswali ndani ya msikiti huku wakiwa wamebanana baadala yake waswali nje ya msikiti.

Amesema hakuna chombo chochote wala taasisi yoyote itakayofanya balaza la Eid katika Mkoa huo kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma hivyo watu wakimaliza kuswali waelekee majumbani.

Pia, katika taratibu za mialiko ya Eid iwe ni mialiko ya mtu mmoja mmoja nasio kundi la watu ili kuepusha misongamano isiyo ya lazima.

Kakulukulu amesema kumi hili la mwisho ni kumi ambalo Mwenyezi Mungu anawaacha huru na moto na pia unapatikana usiku wenye cheo, hivyo waislamu wazidishe kuswali ibada za usiku na wajiandae kutoa dhakatul fitiri ambapo katika Mkoa wa Katavi ni sh 2,500 kwa kila kichwa kama hana anaweza kutoa chakula chenye thamani ya pesa hiyo.

Habari Kubwa