Sheria kandamizi zasababisha kesi za ukatili kufutwa Zanzibar

16Jan 2019
Rahma Suleiman
Zanzibar
Nipashe
Sheria kandamizi zasababisha kesi za ukatili kufutwa Zanzibar

Mkurugenzi wa mashtaka Zanzibar Ibrahim Mzee amesema kuwa kutokana na ukali wa sheria mpya ya mwenendo wa makosa ya jinai imepelekea maombi mengi ya kufuta kesi za udhalilishaji.

Mkurugenzi wa mashtaka Zanzibar Ibrahim Mzee (katikati ) akizungumza na wajumbe wa kamati ya wanawake, habari na utalii wa baraza la wawakilishi. picha mtandao

Aliyasema hayo wakati akizungumza katika kikao cha pamoja na kamati ya maendeleo ya wanawake, habari na utalii ya baraza la wawakilishi

Alisema kwa kipindi cha Julai hadi Disemba mwaka 2018 afisi yake imepokea maombi 11 ya kufutwa kesi kutoka kwa wazazi wa wahanga wa makosa ya kujamiiana.

Alisema idadi hiyo inaweza kuongezeka kwani wazazi wengine huwasilisha maombi hayo siku ambayo kesi inapopelekwa mahakamani.

Habari Kubwa