Sheria sasa kutumia lugha ya Kiswahili

10Apr 2021
Ashton Balaigwa
Morogoro
Nipashe
Sheria sasa kutumia lugha ya Kiswahili

OFISI ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, imesema kuanzia sasa Sheria mpya zitakazotungwa na kuwasilishwa bungeni zitaanza kutumia Lugha ya Kiswahili ili kuleta ulewa kwa wananchi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Bunge la Jamhuri ya Muungano.

Sambamba na hilo imesema tayari imeanza mchakato wa  kuzitafsili sheria kuu 450  zilizotungwa kwa lugha ya Kingereza ili  zitumike kwa lugha ya Kishwahili ikiwa ni utekelezaji wa agizo hilo.

Mwandishi Mkuu wa Sheria kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Onorius Njole,alisema hayo  wakati wa Mkutano wa  Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo iliyofanyika mjini Morogoro.

Alisema kuwa mchakato huo wa kuzitafrisili sheria zilizopo ambazo zilitungwa kwa lugha ya kiingereza utakamilika mwezi Disemba mwakani na baada ya kukamilika kwake utafuata mchakato wa kuzitafsili sheria ndogo 30,000  zilizotungwa  na taasisi,mamlaka za serikali pamoja na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Habari Kubwa