Sheria ya ujazo yasisitizwa kupambana na soko la kimataifa

16May 2019
George Tarimo
IRINGA
Nipashe
Sheria ya ujazo yasisitizwa kupambana na soko la kimataifa

WAKALA wa vipimo vya Ujazo na uzito Mkoani Iringa wamewataka wafanyabiashara na wamiliki wenye viwanda mkoani humo kuzalisha bidhaa zenye ubora pamoja na kuzingatia sheria ya ujazo ili kupambana na soko la kimataifa.

 

Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa Wakala wa Vipimo Mkoa wa Iringa Samweli Simon, wakati wa ukaguzi maalumu viwandani ambapo amesema wanatakiwa kuzalisha bidhaa bora,ambazo zimejazwa katika ujazo unaotakiwa, bidhaa ambazo zinaweza kushindana na soko la kimataifa.

 

Meneja huyo alisema kuwa inapotokea anapunja ujazo kutokana na matatizo ya kipimo chake ni kosa na hivyo anatakiwa kurekebisha na kama amepunja kwa lengo la kuwaibia wananchi ni kosa la jinai na kwa mujibu wa sheria ya vipimo anatakiwa kutozwa faini ya hapo kwa papo isiyopungua shilingi 100,000 na isiyozidi Milioni 20 na iwapo kama wameona ni suala ambalo anaweza kupelekwa mahakamani na kama kosa ni la kwanza faini yake haipungui 300,000 na isiyozidi Milioni 50.

Alisema kuwa wenye viwanda wanatakiwa kuona umuhimu wa kuhakikisha vipimo vyao vinatoa vipimo sahihi lakini pia katika biashara na kukuza uchumi wan chi wanatakiwa kujuwa wanawalaji hata nje ya Taifa hivyo wakikosea vipimo wanaweza kupoteza ubora wa bidhaa na taifa kukosa fedha za kigeni.

Naye Ayubu Kibabage ambaye ni msimamizi wa kiwanda cha Iringa Foods Privalages alisema zoezi hilo limesaidi kwa kiasi kikubwa kumlinda mlaji huku akiwataka wazalishaji wengine kuzingatia sheria ya vipimo.

Kibabage alisema kuwa “Hiki kinachofanywa na shirika la vipimo kina manufaa kwa watumiaji na viwanda vilevile kwa sababu kwetu sisi tunataka tuuze kwa vipimo vilivyo sahihi ili viingie sokoni na kwa mlaji kinamnufaisha pale ambapo anataka kununua kile kitu kwa mujibu wa maandishi yaliyopo kwenye bidhaa.”alisema

Eva Ikula ambaye ni ofisa vipimo wa mkoa wa Iringa alisema kuwa baadhi ya wananchi hawana uelewa juu ya kugagagua ujazo na uzito.

Habari Kubwa