Akitoa msaada huo leo mjini Masasi, Mratibu wa Shirika hilo Tawi la Masasi, Hussein Mchomolo amesema kuwa Shirika hilo limeamua kutoa msaada wa baiskeli kwa mtoto huyo baada ya kuguswa na uhitaji wa kifaa hicho.
Amesema kuwa Shirika hilo limekuwa likifanya hivyo kwa watoto mbalimbali ambao ni walemavu na wanauhitaji wa misaada ya kijamii ili na wao waweze kujihisi kama watu wengine ambao sio walemavu.
Mchomolo, amesema kuwa Shirika hilo linafanya kazi hizo za kijamii katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Dar es saalam , Ruvuma , Lindi na Mtwara.