Shyrose Bhanji aeleza hisia zake kifo cha mwanafaunzi NIT

18Feb 2018
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe Jumapili
Shyrose Bhanji aeleza hisia zake kifo cha mwanafaunzi NIT

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shyrose Bhanji ameeleza hisia zake juu ya tukio la kifo cha mwanafunzi wa chuo cha NIT, Aqulina Akwilini, kilichotokea kwa kupigwa risasi na walipokuwa wakiwatawan ya wafuasi wa chadema juzi na kumpata mwanafunzi huyo aliyekuwa ndani ya daladala.

Shyrose Bhanji.

Shyrose amesema kuwa Chama chake cha CCM na serikali haviwezi kukwepa lawama za tukio hilo, Bhanji amesema  kuwa tukio hilo linamfanya ashindwe kula wala kulala kwani ameuawa kikatili na hakua na hatia yoyote ile.

“Serikali ya chama changu CCM haiwezi kukwepa lawama kwa namna yoyote ile kufuatia kupigwa risasi kwa binti ambaye hakuwa na hatia hata kidogo. Imekuwa ni siku mbaya sana kwangu; nimeshindwa kula na nashindwa kupata usingizi kutokana na kifo cha huyu binti. Nafsi yangu inanisuta. Mungu wangu naomba unisaidie,“ ameandika Bhanji kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Habari Kubwa