Siku ya Usafi Duniani Kanda ya Kaskazini yahitimishwa Mto Ngarenaro

03Oct 2021
Na Mwandishi Wetu
Arusha
Nipashe Jumapili
Siku ya Usafi Duniani Kanda ya Kaskazini yahitimishwa Mto Ngarenaro

​​​​​​​BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na Ofisi ya Bodi ya maji Bonde la Pangani mkoani Arusha pamoja na Alliance Francie Arusha wamehitimisha Siku ya Usafi Duniani kwa kufanya usafi katika Mto wa Ngarenaro.

"Zoezi tulilolifanya siku ya tarehe 18 Septemba, 2021 katika Mto Naura inaonekana kabisa Mto Ngarenaro umechafuka kwa kiasi kikubwa sana na hii inaonekana wazi inachangiwa na tabia za watu lakini pia na miundombinu." amesema Afisa Mazingira wa NEMC Kanda ya Kaskazini Francis Nyamhanga.

Kwa upande wake, Muwakilishi toka Ofisi ya Bodi ya Maji Bonde la Pangani mkoani Arusha Hezron Phillipo, amesema uchafuzi wa vyanzo vya maji unatokana na jamii kutozingatia mita 60 toka katika vyanzo vya maji badala yake imekuwa ikiendesha shughuli za kijamii pembezoni mwa mito na vyanzo vya maji.

Naye, Afisa Mawasiliano na Masoko wa Shirika la Alliance Francie Arusha Rehema Hamza Kiwanga, amesema kupitia mradi wao wa Green Ecolog unaotekelezwa na shirika hilo wamejikita katika utunzaji wa mazingira kwa ustawi wa mito na vyanzo vya maji.

Habari Kubwa