Simbachawene aagiza trafiki wenye vitambi kupangiwa kazi nyingine

23May 2020
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Simbachawene aagiza trafiki wenye vitambi kupangiwa kazi nyingine

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Geogre Simbachawene, amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,  IGP Simon Sirro, kuwaondoa askari wote wa Usalama Barabarani wenye vitambi na kuwapangia kazi nyingine kwani wamekosa sifa. 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Geogre Simbachawene.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa Kongamano ya Usalama Barabarani lililofanyika mjini Dodoma."Wapo Trafiki wanastahili kuondolewa kwa kukosa sifa ya kuwa trafiki!! Kwa mfano wa Trafiki wa Gairo wana vitambi! askari anakuwaje na kitambi?"- amesema Simbachawene na kuongeza kuwa;

"Wapo askari wa usalama barabarani ambao wamegeuza 'crown', sare nyeupe na kofia kudai rushwa kutoka kwa bodaboda, malori na kirikuu!! naelekeza trafiki kufanya kazi kwa weledi! tuache kusimamia sheria kwa mazoea!”

Amesema kuwa ajali zimekuwa zikigharimu serikali kurekebisha miundombinu, kufanya maokozi, kupoteza nguvu kazi ya taifa "Ajali hizi zimekuwa zikiigharimu serikali kurekebisha miundombinu, kufanya maokozi na kupoteza nguvu kazi ya taifa.

"Serikali kupitia wizara yangu ipo katika mchakato wa kurekebisha Sheria ya Usalama Barabarani 1973, ili iweze kuendana na mahitaji ya sasa" amesema Simbachawene

Amesema kuwa wapo madereva wanaendesha magari wakiwa wamelewa; wapo watembea kwa miguu wanavuka barabara wakiwa wamelewa; wapo madereva wanaendesha mwendokasi hatarishi katika maeneo ya makazi ya watu au yasiyoruhusiwa na alama za barabarani.

"Kongamano la usalama barabarani ni siku muhimu sana ya kukumbushana kuhusu masuala mbalimbali ya usalama barabarani. Masuala hayo ni pamoja na kuwakumbusha madereva juu ya kuwa waangalifu na kuzingatia sheria" amesema Simbachawene

Chanzo:

Habari Kubwa