Waziri Simbachawene alieleza kuwa kitendo cha wageni hao kukamatwa maeneo mbalimbali ndani ya nchi wakiwa wameshavuka mipaka ni kutokana na kuwepo na mawakala wanaofanikisha wahamiaji hao kuingia nchini.
Akizungumza wakati akifungua mafunzo ya uongozi kwa maofisa na askari wa Idara ya Uhamiaji katika kambi mpya ya mafunzo ya Boma Kichaka Miba iliyopo wilayani Mkinga, Mkoa wa Tanga, aliwaambia watawashughulikia askari wote wanaokaa katika mikoa ya mipakani ambayo wahamiaji hao wanaingia kwa mara ya kwanza.
Soma zaidi: https://epaper.ippmedia.com