Simbachawene azionya Jumuiya chini ya Wizara yake zitakazokiuka sheria

10Jun 2021
Na Mwandishi Wetu
Dodoma
Nipashe
Simbachawene azionya Jumuiya chini ya Wizara yake zitakazokiuka sheria

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, amesema Serikali haitasita kuzichukulia hatua kali kwa Jumuiya zote zilizopo katika Wizara yake ambazo zitaonekana kukiuka sharia na taratibu katika kujiendesha.

George Simbachawene.

Waziri Simbachawene amesema hayo leo leo June 10, 2021 Jijini Dodoma katika kikao alichoketi pamoja na Shirikisho la Wamiliki na Mameneja wa Shule na Vyuo binafsi nchini (TAMONGSCO), huku akitoa msisitizo kwa wale ambao wamekuwa na utaratibu wa kuleta vurugu na kuzivuruga Jumuiya kuwa Wizara yake itachukua hatua kali ambapo amedai ikiwezekana hata pingu zitatumika.

“Ikibidi pingu itatembea haiwezekani mtu akawa anavunja sheria halafu anaangaliwa tu na mimi nitatuma vyombo vya kufanya uchunguzi na tutachukua hatua kali kwa sababu wamekiuka sheria za nchi."

“Songeni mbele atakaeleta shida mimi ndio nitakaeshughulika nae na salamu hizi ziwafikie jumuiya hizi zinaundwa kwa mujibu wa sheria za nchi haiwezekani watu wakawa wanafanya fanya masihara tutachukua hatua kali kwa wale ambao wanavuruga vuruga.” Amesema Waziri Simbachawene.

Habari Kubwa